Japan inatumia roboti kuwahudumia wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona waliowekwa karantini katika hoteli tofauti mjini Tokyo. Na nchini Ujerumani, kumezinduliwa App inayompa fursa shabiki wa soka kushangilia timu yake kama vile yuko kiwanjani wakati akiwa nyumbani.