1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robo fainali ya ligi ya mabingwa kuanza

13 Aprili 2015

Mashabiki wa soka mjini Madrid pamoja na Ulaya nzima na kwingineko watakuwa mbele ya televisheni zao kushuhudia mchezo wa robo fainali mkondo wa kwanza katika kombe la mabingwa wa Ulaya

https://p.dw.com/p/1F7HE
Spanien Fussball Club Atlético de Madrid gegen Real Madrid CF
Picha: Gonzalo Arroyo Moreno/Getty Images

Mabingwa watetezi Real Madrid watashuka dimbani na Atletico Madrid, katika mchuano ambao mashabiki wanatumai utakuwa wa kusisimua kama fainali ya kombe hilo mwaka jana.

Real iliwashinda mahasimu wao hao katika jiji hilo kwa mabao 4-1 mjini Lisbon Mei mwaka jana , lakini idadi ya magoli haielezi hadithi kamili wakati Atletico ilibakiza dakika chake tu kutawazwa mabingwa siku hiyo kabla ya Sergio Ramos kusawazisha katika dakika za majeruhi.

Mpambano kama huo unatarajiwa katika michezo yao miwili ya robo fainali kwa mujibu wa kocha wa Atletico Diego Simeone.

Mpambano mwingine ni kati ya Juventus Turin na AS Monaco. Kocha wa Juve Massimiliano Allegri amewahakikishia mashabiki kwamba Monaco itakuwa tofauti, lakini kila kitu kinawezekana.

Bayern Munich inacheza kesho dhidi ya Prto ya Ureno. Mchezo mwingine ni kati ya Paris St Germain dhidi ya Barcelona.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf, Saumu