1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH : Syria yashinikizwa kuondoka Lebanon

4 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZi

Saudi Arabia hivi sasa inaishinikiza Syria kujitowa Lebanon.

Mwana mrithi wa ufalme wa Saudia Prince Abdullah amekutana na Rais Bashar al Assaad wa Syria kwa mazungumzo ya mzozo huo huku shinikizo la kimataifa likizidi kuongezeka kutaka Syria ikomeshe udhibiti wake wa kisiasa na kijeshi kwa Lebanon. Serikali ya Syria imekuwa ikishutumiwa kwa kuhusika na mauaji ya mwezi uliopita ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri mjini Beirut.Maafisa wa Marekani wanasema serikali ya Marekani na Umoja wa Ulaya wanafikiriwa kuiwekea Syria vikwazo vya pamoja.

Wakati wa ziara yake nchini Yemen Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani pia ameitaka serikali ya Damascus kuipa Lebanon nafasi ya kuwa na uhuru.