1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Mfalme wa Saudi Arabia aihimiza Syria iondoe majeshi yake Lebanon.

4 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZq

Utawala wa Saudi Arabia umeongeza sauti yake kuunga mkono juhudi za kuishinikiza Syria iondoe majeshi yake kutoka Lebanon mara moja.

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia alimueleza hayo rais wa Syria Bashar al Assad katika mkutano wao huko Riyadh ambako rais wa Syria alikwenda kwa mazungumzo ya dharura na mfalme Abdullah.

Jamii ya kimataifa imepaaza sauti kwa Syria iyaondoe majeshi yake alfu kumi na nne yaliyopo Lebanon na serikali hiyo ya Damascus inalaumiwa katika mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri mwezi uliopita huko Beirut.

Kansela wa Ujerumani Gerhard Shröder aliye ziarani katika nchi za kiarabu alipo kuwa Yemen, alitoa wito wa kuitaka Syria iyaondoe majeshi yake kutoka Lebanon ili kuipa nchi hiyo uhuru wake wa kujitawala katika mswala yake ya ndani.