1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH :Iran yalaumiwa na Saudi Arabia kwa msimamo wake wa nyuklia

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUu

Saudi Arabia imeilaumu Iran kwa msimamo wake mkali juu ya mpango wake wa nyuklia unaosababisha mvutano na jumuiya ya kimataifa.

Lawama hizo zimetolewa na Mfalme Abdullah wakati wa mazungumzo yake na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani. Mfalme huyo amesema kuwa msimamo wa Iran ni wa makosa japo nchi yake itaendelea kuwa rafiki wa nchi hiyo.

Wakati huo huo mjumbe wa Iran juu suala la nykulia Agha Zadeh amesema kuwa wawakilishi wa kibalozi wa nchi za magharibi wataruhusiwa kuvitembelea vituo muhimu vya nykulia vya nchi yake.