Ripoti ya Wikileaks juu ya Unyanyasaji Iraq.
23 Oktoba 2010Matangazo
Marekani ilitambua lakini ilishindwa kuchunguza visa vya unyanyasaji wa wafungwa kulikofanywa na maafisa wa usalama wa Iraq.
Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu nyaraka laki nne zilizofichuliwa kuhusu vita vya Iraq.
Mtandao wa wikileaks umetoa nyaraka hizo kwa vyombo kadhaa vya habari hapo jana usiku likiwemo gazeti la Ujerumani la Der Spiegel.
Nyaraka hizo zinaonekana kuonyesha kuwa mamia ya raia wa Iraq waliuawa na wanajeshi wa Marekani katika vizuizi tangu kuvamiwa kwa nchi hiyo mwaka 2003.
Hata hivyo Marekani imekosoa kufichuliwa kwa kiasi kikubwa kwa taarifa hizo kuliko ilivyokuwa awali na kusema kuwa uhalifu wowote uliojulikana uliripotiwa kwa maafisa husika.