1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya NATO yatia shaka juu ya mafanikio ya vita Afghanistan

Sekione Kitojo1 Februari 2012

Jeshi la Marekani limesema katika ripoti kuwa kundi la Taliban likiungwa mkono na Pakistan ,linajitayarisha kuchukua udhibiti wa Afghanistan baada ya majeshi yanayoongozwa na NATO kuondoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/13uNI
Taliban soldiers with guns stand guard in Bamiyan, Afghanistan, in this undated but recent photo. Opposition leaders claimed Tuesday, June 5, 2001 at least 100 Taliban fighters died in the fighting Monday and Tuesday and that their soldiers had captured the strategic Yakawlang district in central Bamiyan province. The Taliban Islamic militia controls 95 percent of the country and is fighting the opposition to capture the remaining five percent. (AP Photo/Amir Shah)
Wapiganaji wa kundi la Taliban nchini AfghanistanPicha: AP

Je sera za NATO zimeshindwa?

Taarifa hiyo ya jeshi la Marekani imeongeza uwezekano wa hali ya kushindwa kwa sera za mataifa ya magharibi baada ya vita vilivyotumia gharama kubwa.

Luteni kanali Jimmie Cummings , msemaji wa jeshi la kimataifa la usaidizi wa kuleta amani linaloongozwa na NATO, amethibitisha kuwapo kwa waraka, ambao umeripotiwa na gazeti la Uingereza la Times na pia kituo cha televisheni cha BBC. Lakini amesema huo si uchunguzi wa kimkakati.

Waraka huo wa siri ni mjumuisho wa maoni ya Wataliban ambao wako jela , amesema. Sio tathmini , na wala haikulengwa kufikiriwa kuwa ni tathmini.

Hata hivyo, waraka huo unaweza kutafsiriwa kuwa ni tathmini mbaya kuhusiana na vita hivyo, ambavyo hivi sasa vinaelekea kuingia katika mwaka wa kumi na moja , katika vita vyenye lengo la kulizuwia kundi la Taliban kurejea madarakani.

Unaweza pia kuonekana kama kukubali kushindwa na kunaweza kuimarisha mtazamo wa Wataliban wenye msimamo mkali kuwa hawana haja ya kufanya majadiliano na Marekani na serikali ya rais Hamid Karzai ambayo haina umaarufu wakati kundi hilo limo katika nafasi imara.

Afghan President Hamid Karzai listens to U.S. Vice President Joe Biden, unseen, during a press conference in Kabul, Afghanistan in this Jan. 11, 2011 file photo. Karzai said Saturday June 18, 2011 that Afghanistan and the United States are in peace talks with Taliban fighters, in the first official acknowledgment of such negotiations to end the decade-long war. Officials at the U.S. Embassy in Kabul could not be immediately reached for comment Saturday. (Foto:Musadeq Sadeq, File/AP/dapd)
Rais wa Afghanistan Hamid KarzaiPicha: AP

Pakistan yahusika.

Jeshi la Marekani limesema katika waraka huo kuwa shirika la ujasusi la Pakistan ISI linasaidia kundi la Taliban katika mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya majeshi ya kigeni.

Madai hayo yamezua jibu kali kutoka kwa msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Pakistan Abdul Basit. Huu ni upotoshaji, kusema kweli, ameliambia shirika la habari la Reuters. Hatutaki kabisa kuingilia mambo ya ndani ya Afghanistan.

Gazeti la Times limesema kuwa ripoti ambayo ni ya siri mno ilitayarishwa na jeshi la Marekani katika kituo cha jeshi la anga cha Bagram nchini Afghanistan kwa ajili ya maafisa wa ngazi ya juu wa NATO mwezi uliopita.

Maeneo makubwa ya Afghanistan yamekabidhiwa kwa majeshi ya usalama ya Afghanistan, ambapo kikosi cha mwisho cha jeshi la kigeni kikitarajiwa kuondoka nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014.

Waafghani wanashaka

Lakini Wafghani wengi wana shaka iwapo jeshi lao la usalama litaweza kuchukua udhibiti kamili wa nchi hiyo , ambayo imekumbwa na machafuko kadha , mara tu baada ya majeshi ya kigeni kuondoka nchini humo. Waraka huo unaweza kuwaacha baadhi ya viongozi nchini Marekani wakijiuliza iwapo vita nchini Afghanistan vilikuwa vinastahili gharama kubwa , kwa maisha ya binadamu na fedha.

Uhusiano waporomoka zaidi

Pakistan inatathmini upya uhusiano wake na Marekani ambao umeaathirika kutokana na wimbi la mambo kadha tangu pale Marekani ilipofanya shambulio bila kuiarifu serikali ya Pakistan na kuuwawa kwa Osama bin Laden katika ardhi ya Pakistan Mei mwaka jana na kusababisha kudhalilika kwa majenerali wakubwa nchini humo.

Shambulio la anga la NATO la hapo Novemba 26 katika mpaka ambapo wanajeshi 29 wa pakistan wameuwawa limezidisha mzozo huo , na kusababisha Pakistan kufunga njia za kupeleka vifaa vya jeshi la NATO ndani ya Afghanistan.

An Afghan military helicopter fires on a building which is occupied by Taliban insurgents during a coordinated assault in Kabul, Afghanistan, on Tuesday, Sept. 13, 2011. Taliban insurgents fired rocket-propelled grenades and assault rifles at the U.S. Embassy, NATO headquarters and other buildings in the heart of the Afghan capital Tuesday while suicide bombers struck police buildings. The U.S. Embassy and NATO reported no casualties. (Foto:Musadeq Sadeq/AP/dapd)
Ndege ya jeshi la NATO katika harakati za mapambano dhidi ya TalibanPicha: dapd

Pakistan inaonekana kuwa muhimu kwa juhudi za Marekani kuipa Afghanistan uimara, hali ambayo mataifa ya kigeni moja baada ya jingine yameshindwa katika historia ya misukosuko katika nchi hiyo.

Pakistan inasema kuwa Marekani inapaswa kuyaleta pamoja makundi yote yenye silaha katika hatua za kuleta amani na inahofia kuondoka kwa majeshi ya NATO mwaka 2014 kuwa ni hatua ya haraka mno , na huenda ikaliingiza eneo lote katika hali ya ghasia ambayo ilijitokeza mara baada ya Urusi ya zamani kujitoa nchini humo mwaka 1989.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman.