1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Watu milioni 35 ni wakimbizi Afrika sababu ya mizozo

26 Novemba 2024

Ripoti ya waangalizi wa kimataifa iliyotolewa leo Jumanne imesema kwamba mizozo, machafuko na majanga kote barani Afrika yameiongeza mara tatu idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao barani humo.

https://p.dw.com/p/4nQkS
Kambi ya wakimbizi Chad
Kambi ya wakimbizi ChadPicha: Sam Mednick/AP

Ripoti ya waangalizi wa kimataifa iliyotolewa leo Jumanne imesema kwamba mizozo, machafuko na majanga kote barani Afrika yameiongeza mara tatu idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao barani humo katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Kulingana na ripoti ya shirika linalofuatilia mienendo ya watu kulazimika kuyahama makazi yao ndani ya nchi zao, IDMC, kufikia mwisho wa mwaka uliopita, bara la Afrika lilikuwa na watu milioni 35 wanaoishi nje ya makazi yao katika nchi zao.

Mkuu wa shirika hilo Alexandra Bilak amesema idadi hiyo ni karibu nusu ya idadi jumla ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao ulimwenguni kote. Wengi wao, au watu milioni 32.5, wamekimbia vurugu na  migogoro ya silaha.

Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Nigeria na Somalia - zinawapa hifadhi 80% ya wakimbizi na walioyahama makazi yao.