1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yawa muagizaji wa tatu wa silaha duniani, 2022

13 Machi 2023

Taasisi ya utafiti wa masuala ya amani duniani iliyoko Stolkholm, Sweden ya SIPRI, imesema biashara ya silaha kwa ujumla duniani imepungua, lakini imeongezeka kwa kiwango kikubwa barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4Ob02
USA weiter an der Spitze bei Waffenexporten/F-35
Picha: picture alliance/dpa/dpa-Zentralbild

Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani (SIPRI) aidha imesema Ukraine imekuwa muagizaji mkuu wa tatu wa silaha duniani mnamo mwaka 2022.

Mtafiti mkuu katika taasisi hiyo ya SIPRI yenye makao yake makuu mjini Stockhom, Sweden na anayehusika na mpango wa uhamisho wa silaha, Pieter Wezeman amesema Ukraine inapokea kiasi kikubwa cha silaha kutoka kwa Mataifa ya Ulaya na Marekani kufuatia uvamizi wa Urusi.

Wezeman amebaini pia kuwa mauzo ya nje ya nchi ya silaha za Urusi ambayo kwa kawaida huwa ni ya juu yamepungua kwa asilimia 31 kati ya mwaka 2013 na 2022.

Hata hivyo usafirishaji wa silaha za Urusi kuelekea China na Misri umeongezeka.