1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tatizo la maji linatishia uzalishaji wa chakula duniani

Sylvia Mwehozi
17 Oktoba 2024

Ripoti mpya iliyotolewa na Tume ya Kimataifa ya Uchumi wa Maji GCEW, inasema kutochukuliwa hatua za kumaliza tatizo la maji, kunaweza kusababisha zaidi ya nusu ya uzalishaji wa chakula duniani kuwa hatarini ifikapo 2050.

https://p.dw.com/p/4ltGO
Wakaazi wa Msumbiji wakichota maji
Wakaazi wa Msumbiji wakichota majiPicha: Chris Huby/Le Pictorium/dpa/picture alliance

Ripoti mpya iliyotolewa na Tume ya Kimataifa ya Uchumi wa Maji GCEW, inasema kutochukuliwa hatua za kutosha za kumaliza tatizo la maji, kunaweza kusababisha zaidi ya nusu ya uzalishaji wa chakula duniani kuwa hatarini ifikapo mwaka 2050. Ripoti hiyo imeonesha kuwa zaidi ya nusu ya uzalishaji wa chakula duniani na takriban watu bilioni 3 wako katika maeneo ambayo hifadhi ya maji inakadiriwa kupungua.

Soma: Siku ya Maji Duniani

Ripoti hiyo pia ilionya tatizo la maji linaweza kusababisha kushuka kwa asilimia nane ya Pato la Taifa kwa wastani, katika nchi zenye kipato cha juu ifikapo mwaka 2050 na hadi asilimia 15 kwa nchi za kipato cha chini. Ingawa maji mara nyingi huchukuliwa kuwa zawadi kubwa ya asili, lakini ripoti hiyo imesisitiza kuwa maji ni rasilimali adimu na ya gharama kubwa kusafirisha.