Ripoti: Dunia ingeweza kuepuka athari mbaya za Covid-19
12 Mei 2021Ripoti hiyo ya jopo linalofuatilia utayari wa kukabiliana na maradhi ya mlipuko imesema msururu wa maamuzi mabaya umechochea janga la Corona kusababisha vifo vya watu 3.3 duniani na kuvuruga uchumi wa ulimwengu.
Kulingana na ripoti hiyo, kushindwa kwa serikali duniani kuweka mifumo thabiti pamoja na viongozi waliopuuza kitisho cha janga la corona kulichangia kwa sehemu kubwa kuanguka kwa imani ya umma kuhusu maelekezo ya wataalamu wa afya.
Ripoti hiyo ambayo imesubiriwa kwa karibu mwaka mmoja imetaka mfumo wa dunia wa kutoa tahadhari kufanyiwa mageuzi makubwa kwa lengo la kuepusha janga kama la Corona kutokea tena.Wimbi la maambukizi ya Covid-19 bado laitikisa India
Jopo hilo limesema msururu wa maamuzi mabaya katika kupambana na Covid-19 umesababisha vifo vya watu wasiopungua milioni 3.3 hadi sasa na kuzorotesha uchumi wa ulimwengu.
Ripoti hiyo imesema taasisi "zilishindwa kuwalinda watu" na viongozi wanaopinga sayansi walididimiza imani ya umma katika kushughulikia swala la afya.
Hatua za mapema juu ya mlipuko ulipogunduliwa huko Wuhan, China mnamo Desemba 2019 "hazikuchukuliwa kwa haraka", huku Februari 2020 ikiwa ndio mwaka uliokuwa na maafa mengi kwa sababu hazikusikia onyo lililotolewa.
Ili kupambana na janga lililopo, IPPPR imetoa mwito kwa mataifa tajiri ulimwenguni kuchangia dozi bilioni moja kwa nchi maskini na kuyafadhili mashirika mapya yanayojitolea kujiandaa kwa majanga mengine.Marekani yakubali kuondolewa ulinzi wa hatimiliki ya chanjo za COVID
Jopo hilo pia limeilamu WHO kwa kuchelewa kutangaza hali hiyo kuwa suala la Dharura la Afya ya Umma lenye wasiwasi wa Kimataifa (PHEIC) mnamo Januari 22, 2020. Badala yake, ilingoja siku nane zaidi kabla ya kufanya hivyo.
Mataifa tajiri ya G7 yalipe asilimia 60 ya dola Bilioni 19 zinazohitajika kufadhili chanjo, upimaji na tiba kupitia mpango wa WHO wa Upatikanaji wa haraka wa Nyenzo za kupambana na Covid.
Shirika la Afya Ulimwenguni WHO na Shirika la Biashara Duniani WTO yanapaswa pia kufikia nchi zinazotengeneza chanjo na watengenezaji kukubali leseni za hiari na uhamishaji wa teknolojia kwa chanjo ya Covid-19.