RIGA : Viongozi wa NATO wakamilisha mkutano wao
29 Novemba 2006Matangazo
Viongozi kutoka nchi wanachama 26 wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO leo wako katika kikao cha siku ya pili na ya mwisho cha mkutano wa viongozi kwa kulenga masuala ziada ya Afghanistan.
Majadiliano yatakita juu ya wito wa kuwa na Kikosi cha Dharura cha NATO NRF,kutanuwa umoja huo,ushirikiano wa karibu na washirika wa NATO wasio wanachama na taarifa juu ya shughuli za umoja huo kwa dira yake ya muda mrefu.
Viongozi hao wa NATO pia watajadili lengo la muda mrefu la NATO kuugeuza umoja huo kuwa ule wenye ufanisi dhidi ya changamoto mpya kwa ajili ya karne ya 21 kama vila ugaidi na silaha za maangamizi ya umma.