RIGA : NATO yaidhinisha mustakbali wao
29 Novemba 2006Matangazo
Viongozi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO leo wameidhinisha hati muhimu kwa ajili ya mustakbali wa umoja huo wa kijeshi na kuweka msingi kwa nchi wanachama kuendeleza vikosi vyao kuweza kukabiliana na vitisho vya usalama katika kipindi cha muongo mmoja ujao.
Licha ya kichwa chake cha habari cha moyo mzito Muongozo Kabambe wa Kisiasa unaunda sehemu ya taarifa ya shughuli za NATO na kutowa msingi kwa umoja huo ulioanzisha wakati wa enzi ya Vita Baridi kwenda na wakati kupambana na vitisho vya usalama viliopo hivi sasa.
Katika mkutano huo wa NATO umoja huo pia umezipatia Serbia,Bosnia na Montenegro nafasi za hatua za kwanza kuelekea kujiunga na umoja huo.