Ripoti mpya ya taasisi ya Utafiti kwa elimu ya Demokrasia ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam -REDET- imesema uchaguzi mkuu wa Tanzania wa 2020 haukuwa na wigo sawa wa ufanyaji siasa na hivyo kuathiri kwa kiwango kikubwa ushiriki wa upinzani katika uchaguzi huo. Marcel Hamduni ni mchambuzi wa siasa nchini humo na anaitathmini ripoti hiyo.