Real, Manchester City zatinga nusu fainali
13 Aprili 2016Baada ya kufunga mabao mawili yaliyofuatana haraka katika kipindi cha kwanza, mshambuliaji huyo Mreno alikamilisha kazi kwa mkwaju wa freekick katika kipindi cha pili, na kuipa Madrid ushindi wa tatu bila. Katika mchezo wa awali Wolf-Sburg walishinda 2-0 na hivyo Madrid imesngambele kwa jumla ya mabao 5-2
Katika mchuano mwingine wa jana usiku Manchester City ilishinda moja bila dhidi ya Paris Saint-Germain na kuwabandua nje mabingwa hao wa Ufaransa. Wakicheza katika uga wao wa Etihad City walifanikiwa kufunga bao safi sana na la ushindi katika dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji De Bruyne. Katika mchuano wa kwanza, timu hizo zilizoka sare ya 2-2 na hivyo City imefuzu kwa jumla ya mabao 3-2
Leo ni zamu ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watakaopiga ugenini dhidi ya Benfica ya Ureno wakiwa na faida ya bao moja sifuri kutokana na mkondo wa kwanza. Mabingwa watetezi Barcelona watakuwa nyumbani kwa Atletico Madrid wakiwa kifua mbele kwa mabao mawili kwa moja. Droo ya nusu fainali itaandaliwa Ijumaa.
Mandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Daniel Gakuba