Real Madrid yaitupa nje Bayern Munich
19 Aprili 2017Mchezo huo uliopangwa kuchezwa siku ya Jumanne uliahirishwa baada ya kutokea shambulio la mabomu dhidi ya basi lililowachukua wachezaji wa Dortmund na hivyo mechi kufanyika siku iliyofuata ya Jumatano.
Mchezo mwingine ni kati ya FC Barcelona ikipambana na Juventus Turin ya Italia ambapo timu hiyo ya jimbo la Catalan ina kibarua kigumu kuweza kubadilisha matokeo ya mchezo wa kwanza ya mabao 3-0. Barcelona iliweza kubadilisha matokeo ya kushindwa kwa mabao 4-0 dhidi ya Paris Saint Germain katika awamu ya timu 16 katika Champions League msimu huu na kushinda kwa maboa 6-3.
Real Madrid ya Uhispania ilifanikiwa kuiondoa Bayern Munich ya Ujerumani katika michuano ya kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, Champions League, kwa ushindi wa mabao 4-2 ambapo mshambuliaji nyota wa timu hiyo Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu.
Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 100 katika Champions League, na ni mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika michezo ya robo fainali mbili katika kinyang'anyiro hicho, baada ya kufanya hivyo msimu uliopita.
Klabu nyingine ya Uhispania, Atletico Madrid, ilifanikiwa pia kuingia katika nusu fainali ya kombe hilo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na mabingwa wa England Leicester City na kupita kwa jumla ya mabao 2-1 katika michezo miwili ya robo fainali.