1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid, Wolfsburg zashinda katika Champions League

18 Februari 2016

Real Madrid na Wolfsburg zimeweka mguu mmoja kwenye hatua ya robo fainali ya Champions League baada ya kupata ushindi ugenini katika mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 za mwisho

https://p.dw.com/p/1Hx6h
UEFA Champions League AS Rom Real Madrid
Picha: Getty Images/P.Bruno

Real Madrid ambao wanashikilia rekodi ya kushinda Champions League mara kumi waliwabwaga AS Roma wa Italia mabao mawili kwa sifuri kupitia magoli ya Cristiano Ronaldo na Jese, katika kile kilichokuwa ni mpambano wa kwanza kwa kocha Zinedine Zidande katika dimba hilo.

Balo la Ronaldo huenda lilikuwa jibu tosha kwa walioikosoa rekodi yake ya ufungaji wa magoli katika mechi za ugenini msimu huu, swali ambalo aliulizwa katika mkesha wa mchuano huu, na kumfanya ajibu kwa hasira na kuondoka kwenye kikao cha waandishi wa habari.

Wolfsburg ilipiga hatua kubwa ya kutinga awamu ijayo baada ya mabao mawili ya Julian Draxler na mshambuliaji Max Kruse kuipa ushindi wa 3-2 dhidi ya klabu ya Ubelgiji Gent, ambao walijibu kupitia wachezaji Sven Kums na Kalifa Coulibaly.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Isaac Gamba