1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid kumenyana na Juventus

12 Mei 2017

Real Madrid  sasa  imo  njiani  kuwa  timu  ya  kwanza  katika  bara la  Ulaya  kutetea  taji  lao  la Champions League  baada  ya  kukata tikiti  yao  katika  fainali dhidi  ya  Juventus Turin  mjini  Cardiff

https://p.dw.com/p/2ctBt
Fußball - UEFA Champions League Real Madrid vs Juventus Turin
Picha: Reuters/Paul Hanna

Ni  mara  ya  tatu  kwa  Real Madrid  kuingia  katika  fainali  katika muda  wa  miaka  minne, ambayo  imefikia  licha  ya  ushindi  wa mahasimu  wao Atletico  Madrid  wa  mabao 2-1 jana  Jumatano.

Real Madrid  imevuka  kwa  ushindi  wa  jumla  wa  mabao  4-2. Real Madrid  iliwashinda  mahasimu  wao hao  kutoka  mjini  Madrid katika  fainali  ya  mwaka  jana  na  pia  mwaka  2014, na  pia iliwatoa  katika  awamu  ya  robo  fainali  mwaka  2015.

Katika nusu fainali ya kwanza,  Juventus Turin  iliishinda  AS Monaco. Wataliani  walionesha  uwezo  wao  mkubwa  katika mchezo  huo  ambao  ulipigiwa  upatu  kuwa  ni  kati  ya  uwezo  wa ulinzi  dhidi  ya  uwezo  wa  ushambuliaji na  kushinda  kwa  mabao 2-1.

Mabao  ya  Mario Mandzukic  na  Dani Alves  yaliweza  kuua  uwezo wa  Monaco  katika  kipindi cha  kwanza. Juventus  ina  matumaini ya  kushinda  taji  hilo  katika  muda  wa  miaka  21  mwezi  ujao mjini  Cardiff.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Sekione Kitojo