1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid klabu tajiri zaidi ulimwenguni

16 Julai 2015

Habayi hizo ni kwa mujibu wa jarida maarufu la biashara la Forbes. Kilabu hiyo ya Uhispania ina thamani ya pauni bilioni 2.08

https://p.dw.com/p/1G024
Cristiano Ronaldo Fußballspieler 2009
Picha: picture-alliance/dpa

Timu ya soka ya Marekani Dallas Cowboys na ile ya New York Yankees zilichukua nafasi ya pili kwa pamoja zikiwa na thamani ya pauni bilioni 2.04.

Mahasimu wakubwa wa Real Madrid Barcelona wamerodheshwa katika nafasi ya nne wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.02.

Kilabu ya Manchester United iko katika nafasi ya tano kutoka nafasi ya tatu mwaka uliopita.

Nafasi nyengine zilizosalia katika kumi bora zinachukuliwa na timu za michezo nchini Marekani.

Timu nyengine za ligi ya Uingereza ni Manchester City iliyonyakua nafasi ya 29 ikiwa na thamani ya pauni milioni 890, Chelsea ikiwa na thamani ya pauni milioni 877 inachukua nafasi ya 31 na Arsenal yenye thamani ya pauni milioni 839 imeorodheshwa katika katika nafasi ya 36 ulimwenguni.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Josephat Charo