1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid guu moja ndani ya nusu fainali Champions League

7 Aprili 2021

Liverpool wana kibarua kigumu cha kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kufungwa 3-1 na Real Madrid jana Jumanne.

https://p.dw.com/p/3rf3j
Fußball Champions League | Real Madrid - Liverpool
Picha: Gabriel Bouys/AFP/Getty Images

Liverpool wana kibarua kigumu cha kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kufungwa 3-1 na Real Madrid jana Jumanne.

Licha ya kipigo hicho, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana imani kuwa timu yake ina uwezo wa kulipiza kisasi na kugeuza matokeo hayo katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki ijayo ugani Anfield.

Mabao ya Real Madrid yalitiwa wavuni na Vinicius Junior na Marco Asensio huku Mohamed Salah akiifungia Liverpool bao la ugenini.

Liverpool inahitaji kushinda kombe la Champions League msimu huu ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa michuano hiyo msimu ujao kwani imeshikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya kandanda ya Uingereza, wakati timu nne za kwanza pekee ndizo zitakazofuzu moja kwa moja kwa michuano hiyo.

Alipoulizwa iwapo timu yake ina uwezo wa kuifunga Real Madrid katika mechi ya marudiano, Klopp alisema "Tunahitaji kufanya kila tuwezavyo. Lazima tupambane hadi mwisho."

Katika msimu wa mwaka 2019, Liverpool ilipindua kipigo cha 3-0 mbele ya Barcelona na kufuzu katika hatua ya nusu fainali.