Real Madrid, Atletico Madrid taabani
14 Januari 2016Matangazo
Klabu hizo zimeadhibiwa na Shirikisho la Kandanda la Kimataifa - FIFA kwa kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji kuhusu kununuliwa kwa wachezaji ambao bado ni watoto.
Marufuku hiyo haitaathiri kipindi cha sasa cha kuwasajili wachezaji, ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu.
Atletico Madrid pia imetozwa faini ya Francs 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na dola 898,000 za Kimarekani wakati Real Madrid wakitakiwa kulipa Francs 360,000.
Katika mwaka wa 2014 Barcelona pia walipatikana na hatia ya kosa kama hilo na FIFA na wakapigwa marufuku kuwasaini wachezaji katika vipindi viwili vya ununuzi wa wachezaji katika mwaka wa 2015.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu