1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMalaysia

Razak apoteza ombi la kutathminiwa upya kesi ya rushwa

31 Machi 2023

Mahakama ya juu ya Malaysia imetupilia mbali ombi la waziri mkuu wa zamani Najib Razak la kutaka kesi ya ufisadi ya mabilioni ya dola katika sakata lililosababisha ahukumiwe iangaziwe upya

https://p.dw.com/p/4PXOa
Malaysia | Prozess Najib Razak
Picha: AP Photo/picture alliance

Hatua hii imefikisha mwisho juhudi za kisheria za Najib za kutaka kuupindua uamuzi wa mahakama uliompata na hatia. Jaji ya mahakama ya shirikisho Vernon Ong, amesema kikao cha majaji watano kilipiga kura ambapo wanne walipinga ombi hilo la Razak.

Soma pia: Najib Razak wa Malaysia kukata rufaa hukumu ya ufisadi

Waziri huyo mkuu wa zamani mwenye umri wa miaka 69, hawezi tena kuwasilisha kesi mahakamani kupinga hukumu hiyo ila amewasilisha ombi la kutaka msamaha ambalo iwapo litakubaliwa, huenda likashuhudia kuachiwa kwake mapema kabla ya kutumikia kifungo kamili cha miaka 12 jela.

Lakini wakili wake Shafee Abdullah amesema ipo nafasi ya kuwasilisha kesi nyengine mahakamani ya kupinga hukumu hiyo kwa kuwa mmoja wa majaji hao watano hakukubaliana na uamuzi uliotolewa.