Rasmussen katibu mkuu mpya wa NATO- uwezo na kipaji chake kinahitajika.
30 Julai 2009Mabadiliko katika uongozi wa juu yamefanyika katika jumuiya ya NATO. Katibu mkuu wa zamani wa NATO Jaap de Hoop Scheffer ameondoka. Mrithi wake ni Anders Fogh Rasmussen, ambayeo hadi hivi karibuni alikuwa kiongozi wa serikali ya Denmark. Katika wadhifa huu mwanasiasa huyu ameonyesha uzoefu wa kidiplomasia na uwezo wa uongozi, na kipaji ambacho anataka kukionesha katika muda wake wa uongozi.
Kuna mengi ambayo waziri mkuu wa Denmark Anders Fogh rasmussen ambayo anaweza kushutumiwa, lakini si kweli, kwamba ameushutumu na kuutusi Uislamu ama katika kile kinachoitwa mzozo wa katuni wa mwaka 2005 alishindwa kuushughulikia. Hapa kuna upinzani kutoka kwa Waislamu kuwa nchi za magharibi zina fikra za kikuuzi. Rasmussen wakati ule amekuwa akitetea uhuru wa vyombo vya habari. Hakutaka kusitisha uchapishaji wa vikatuni hivyo katika vyombo vya habari vya Denmark vinavyokosoa dini ya Kiislamu , kwa kuwa hana haki hiyo na kwa kuwa kama kiongozi wa nchi hataki kuingilia uhuru na mawazo ya vyombo vya habari.
Anders Fogh Rasmussen mbali ya kukosolewa sana pamoja na ghasia zilizofanywa na makundi ya watu katika mataifa ya Kiarabu dhidi ya mali za Denmark ameendelea kushikilia msimamo wake.
Hakutetereka na ameonyesha uwezo wa uongozi. Kuhusu hilo amepata heshima. Umoja wa Ulaya na mataifa ya umoja wa NATO yalisimama wakati huo upande wa Denmark. NATO sio tu umoja wa kijeshi, bali pia ni jamii ya maadili, ambapo uhuru wa vyombo vya habari unawekwa juu kabisa.
Madai ya Uturuki , pamoja na washirika wake wa Kiislamu kwamba Rasmussen angepaswa kuomba msamaha na kwamba kwa Waislamu ni muhimu, ni ya upuuzi.
Angerudi nyuma kutokana na mbinyo kuhusiana na lawama hizo ambazo si sahihi, angeonekana kuwa ameshindwa uongozi na sio upande wa pili, kama vile Uturuki ilivyotaka. Katika mkutano wa NATO mwezi wa Aprili hali ilikuwa wazi, kwamba Uturuki na madai yake ilikuwa peke yake. Washirika wengine wote wa NATO walimuunga mkono Rasmussen.
Anders Fogh Rasmussen anaweza kushutumiwa kuwa alikuwa karibu mno na msimamo wa George W. Bush na kuunga mkono vita vya Iraq. Mtu anaweza pia kukosoa mabadiliko ya haraka katika sera za mambo ya ndani nchini Denmark pamoja na sera ngumu za uhamiaji nchini mwake.
Mtu anaweza kujumuisha ukosoaji huo katika kukataliwa kwa Uturuki kuingia katika umoja wa Ulaya. Ndio sababu hana uadui na Uislamu na kiroho ama kiutu hana mapungufu kwa ajili ya uongozi wa katibu mkuu wa NATO.
Kwa upande mwingine, Rasmussen mwenye umri wa miaka 56 na ambaye hivi sasa yuko katika uongozi wa juu wa umoja huo, kipaji chake kinahitajika, ili kuweza kuweka pamoja maslahi ya mataifa hayo 28 wanachama.
Anapaswa kuleta mkakati mpya na kuielekeza NATO katika njia mpya. Wakati Marekani inataka kuwa kama polisi wa dunia, washirika wa Ulaya mashariki wanamatumaini ya kuilinda Urusi. Ujerumani ikiwa katikati haina uamuzi. Hizi ni changamoto kwa raia huyo wa Denmark, ambaye katika mwaka 2002 katika mkutano wa umoja wa Ulaya mjini Kopenhagen kuhusu upanuzi alitaka kuwa mpatanishi.
Mwamdishi Riegert , Bernd / ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri Mohammed Abdulrahman.
►◄