1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rashford yuko fiti kuivaa Granada

8 Aprili 2021

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford alifanya mazoezi jana Jumanne na yuko kwenye kikosi kilichosafiri hadi Uhispania kwa ajili ya pambano la ligi ya Ulaya Europa League dhidi ya Granada.

https://p.dw.com/p/3rjXx
Grossbritannien | Manchester United | Marcus Rashford
Picha: Imago Images/R. Hart

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford alifanya mazoezi jana Jumatano na yuko kwenye kikosi cha Manchester United kilichosafiri hadi Uhispania kwa ajili ya pambano la ligi ya Ulaya Europa League dhidi ya Granada.

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema Rashford huenda akaanza katika mechi ya leo japo hatacheza dakika zote 90.

Granada inashiriki kwa mara ya kwanza mechi hizo za Ulaya.

Klabu hiyo ya kusini mwa Uhispania licha ya kutokuwa na uzoefu kwenye michuano hiyo, imewabandua miamba kadhaa ikiwemo Napoli ya Italia.

Arsenal kumenyana na Slavia Prague

Britain Soccer Premier League Arsenal vs Chelsea
Picha: Julian Finney/AP/picture alliance

Arsenal inaingia uwanjani Emirates kupambana na Slavia Prague japo mechi hiyo imetawaliwa na kashfa ya ubaguzi wa rangi.

Inadaiwa kuwa beki wa Slavia Prague Ondrej Kudela alimtolea maneno ya kibaguzi mchezaji wa Rangers Glen Kamara katika mechi ya raundi iliyopita.

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA lilimpiga mafuruku Kudela kutoshiriki mechi ya leo dhidi ya Arsenal baada ya kufungua shauri kwa shtaka la ubaguzi.

Polisi ya Scotland pia inachunguza tukio hilo. Hata hivyo, klabu ya Slavia imesema Kudela ni mgonjwa kwa hivyo hatoshiriki mchezo wa leo.

Washika bunduki Arsenal watazikosa huduma za beki shoto Kieran Tierney baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa ligi kuu ya England wiki iliyopita dhidi ya Liverpool.

Mechi nyengine za robo fainali za ligi ya Ulaya zinazikutanisha klabu ya Ajax ya Uholanzi dhidi ya Roma ya Italia wakati Dinamo Zagreb ikimaliza udhia na Villareal.