1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa atangaza, upungufu wa umeme kuwa janga la taifa

10 Februari 2023

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake inapaswa kushughulikia mzozo wa upatikanaji umeme na athari zake kunusuru uchumi wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4NJoN
Südafrika Ramaphosa | Lage der Nation
Picha: GCIS/AP Photo/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza "hali ya janga la taifa" katika uamuzi unaolenga kuongeza kasi ya kushughulikia upungufu mkubwa wa umeme unaolikabili taifa hilo ambalo ni miongoni mwa yale yenye uchumi mkubwa barani Afrika.

Akizungumza kupitia hotuba kwa taifa kiongozi huyo amesema Afrika Kusini inapaswa kushughulikia mzozo wa upatikanaji umeme na athari zake kunusuru uchumi wa taifa hilo linalotegemea viwanda.

Hotuba hiyo mbele ya bunge ilichelewa kwa karibu dakika 45 baada ya wanasiasa wa upinzani kujaribu kuzuia isitolewe.

Uamuzi huo wa kutangaza ukosefu wa umeme wa uhakika kuwa hali ya janga kwa taifa, uawezesha kutolewa kwa fedha zaidi za serikali na rasilimali nyingine kushughulikia kadhia hiyo.

Upungufu wa umeme umesababisha mgao wa nishati hiyo huku athari zake kwenye sehemu za uzalishaji zikitishia kuutumbukiza uchumbi wa Afrika ya Kusini kwenye mkwamo.