RAMALLAH Wajumbe wa NATO wakutana na viongozi wa Palestina
16 Juni 2005Matangazo
Wajumbe wa jumuiya ya mataifa ya kujihami ya NATO, wamekutana kwa mara ya kwanza na mamlaka ya Palestina, katika juhudi mpya ambazo zimeelezewa na muungano huo kwamba hautafuti kuwa na jukumu muhimu katika mpango wa kusaka amani ya mashariki ya kati.
Kiongozi wa ujumbe huo, Ed Kronenburg, amesema lengo la ziara hiyo ni kujenga mahusiano mema na viongozi wa Palestina na kumfahamisha waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Nasser al-Kidwa, juu ya sera za maongozi za shirika la NATO. Katibu mkuu wa NATO, Jaap de Hoop Scheffer, amelitolea wito shirika hilo kuwa tarayi kuunga mkono mkataba wa amani kati ya Israeli na Palestina, iwapo litaalikwa.