1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah: Mgomo wa wafanya kazi wa serekali na waalimu huko Palastina.

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CBIR

Katika maeneo ya Wapalastina, maelfu ya wafanya kazi wa serekali na waalimu wameanza mgomo wa muda usiojulikana, wakitaka walipwe mishahra yao ya miezi kadhaa iliopita. Chama cha wafanya kazi kimesema wanachama wao 165,000 wameufuata mwito huo. Shule nyingi zilibakia jana zimefungwa, ikiwa ni siku ya kwanza ya mhula mpya wa masomo. Huu ni mgomo mkubwa kabisa wa aina hiyo tangu Chama cha Hamas kichukuwe madaraka mwezi Machi mwaka huu. Mishahara haijaweza kulipwa tangu pale nchi fadhili za Magharibi zilipositisha kutoa misaada yao ya fedha, zikilalamika dhidi ya Chama cha Hamas.