1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Kiongozi wa ujasusi katika ukingo wa magharibi, Tawfik Tirawi ajiuzulu.

1 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFRG

Kiongozi wa ujasusi wa kipalestina katika ukingo wa magharibi, Tawfik Tirawi, amejiuzulu. Amesema kujiuzulu kwake ni kwa sababu ya machafuko yanayoendelea katika maeneo yanayokaliwa na wapalestina. Kujiuzulu kwake bado hakujakubaliwa rasmi na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas. Kundi la wanamgambo wa kipalestina lililo na uhusiano na chama tawala cha Fatah, liliyafyatulia risasi makao makuu ya Abbas mjini Ramallah, jana jioni, jambo lililomlazimu kiongozi huyo kuamuru msako katika juhudi za kumaliza machafuko. Wanamgambo hao walifyatua risasi angani katika kiwanja cha makao makuu ya Muqataa, baada ya kuamriwa waondoke kutoka eneo hilo, ambalo wamekuwa wakiishi kwa miezi kadhaa.