1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Yusuf wa Somalia akutana na spika wa bunge

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYNw

NAIROBI

Rais wa Somalia amekuwa na mazungumzo kwenye chumba chake cha hospitali mjini Nairobi Kenya leo hii na mtu ambaye atachukuwa nafasi yake iwapo atashindwa kuiongoza nchi yake hiyo ya Pembe ya Afrika iliokumbwa na machafuko ya umwagaji damu.

Rais Abdulaye Yusuf amekutana na spika wa bunge la Somalia katika hospitali mjini Nairobi ambapo amekuwa akipata nafuu kutokana na mafua makali.Kumekuwepo na taarifa za kutatanisha juu ya kuuguwa kwa Rais Yusuf ambapo taarifa nyengine zinasema alikuwa na ugonjwa wa mapafu.

Balozi wa Somalia nchini Kenya leo amekanusha taarifa za baadhi ya duru za usalama na kidiplomasia kwamba Yusuf yuko mahtuti kuwa ni za uongo.

Rais huyo wa Somalia anatarajiwa kupelekwa Uingereza hivi karibuni kwa uchunguzi wa ini alilopandikizwa.