Rais Yusuf wa Somalia akanusha kwamba alikuwa mahtuti
7 Desemba 2007Matangazo
NAIROBI
Rais Abdulaye Yusuf wa Somalia ameruhusiwa kuondoka hospitalini katika mji mkuu wa Kenya Nairobi leo hii na kukanusha repoti kwamba alikuwa mahtuti.
Rais Yusuf amesema baadhi ya waandishi waliieleza dunia nzima kwamba tayari alikuwa amekufa na kwamba amejionea mwenyewe habari hizo kwenye televisheni lakini yuko hai kama vile wanamvyomuona na anafikiri huo ni ushahidi tosha kwamba waandishi hao ni waongo.
Kulikuwa na repoti za kutatanisha wakati Yusuf alipolazwa hospitali mjini Nairobi hapo Jumanne ilielezwa kuwa alikuwa na ugonjwa wa mapafu wakati kukiwa na wasi wasi kwamba alikuwa akitibiwa kutokana na tatizo la ini alilopandikizwa hapo mwaka 1996.