1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi asema China inasikitishwa na hali ya mbaya ya Gaza

29 Mei 2024

Kituo cha habari cha taifa nchini China, kimeripoti kwamba Rais Xi Jinping amemwambia mwenzake wa Misri AbdelFatah El Sisi kwamba China inasikitishwa sana na hali mbaya inayoshuhudiwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4gQnT
China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping Picha: Yao Dawei/Xinhua News Agency/picture alliance

China imewaalika rais huyo wa Misri pamoja na viongozi wengine wa mataifa ya Kiarabu mjini Beijing kwa mazungumzo ambayo yanalenga kuimarisha msimamo wa pamoja kati ya pande hizo mbili kuelekea hatua ya kutafuta makubaliano ya amani kati ya Israel na kundi la Hamas.

Misri pamoja na Qatar na Marekani zimekuwa kwa miezi, zikihusika kwenye mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu baina ya pande hizo mbili.

Rais wa China ajiandaa kuzungumza na viongozi wa mataifa ya kiarabu mjini Beijing

Rais Xi kesho anatarajiwa kutowa hotuba yake muhimu kwa mataifa ya Kiarabu. China imekuwa na mahusiano mazuri na Israel lakini imekuwa ikiunga mkono juhudi za Wapalestina  kwa miongo na imekuwa ikipigia upatu, mgogoro wa Israel na Palestina utatuliwe kwa suluhu ya kuundwa madola mawili yatakayoishi bega kwa bega.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW