1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais Xi Jinping aanza ziara rasmi nchini Brazil

20 Novemba 2024

Rais Xi Jinping wa China ameanza ziara rasmi nchini Brazil leo baada ya kuhudhuria mikutano miwili ya kilele ikiwemo wa kundi la G20 uliomalizika jana kwenye mji wa mwambao wa Rio de Janeiro.

https://p.dw.com/p/4nDAO
Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Fernando Vergara/AP Photo/picture alliance

Rais Xi Jinping wa China ameanza ziara rasmi nchini Brazil leo baada ya kuhudhuria mikutano miwili ya kilele ikiwemo wa kundi la G20 uliomalizika jana kwenye mji wa mwambao wa Rio de Janenairo.

Xi alilakiwa na mwenyeji wake Rais Luiz Inacio Lula da Silva mjini Brasilia kwa hafla ya kufana iliyojumuisha heshima ya zulia jekundu na gwaride la kijeshi.

Soma pia: Xi, Biden wawasili Peru kwa mkutano wa kilele wa APEC

Shirika la habari la China, Xinhua, limeripoti kwamba Xi atajadili pamoja na Rais Lula masuala ya maendeleo ya kimataifa na kikanda kwa kuzingatia kwamba China ndiyo mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Brazil.

Ziara ya Xi nchini humo inafanyika katika wakati Beijing inajiweka tayari na kipindi kisichotabirika cha mahusiano yake na nchi za magharibi hasa kufuatia ushindi wa Donald Trump kuiongoza tena Marekani.