SiasaUrusi
Medvedev asema jeshi la nchi hiyo litaingia Kiev na Lviv
24 Machi 2023Matangazo
Medvedev amenukuliwa na shirika la habari la RIA Novosti hii leo Ijumaa akisema kwamba hawawezi kuondowa uwezekano wa kuingia kwenye miji hiyo ya Ukraine kuondowa kile alichokiita maambukizo.
Kauli hiyo imekuja wakati hapo jana viongozi wa Umoja wa Ulaya, waliihakikishia tena Ukraine uungaji mkono na kufungua mlango wa kuiwekea vikwazo vipya Urusi.
Soma pia: Rais wa zamani wa Urusi aionya Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuhusu vita vya nyuklia
Katika mkutano mjini Brussels jana, Umoja huo uliahidi kuongeza shinikizo dhidi ya Urusi. Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo, Ursula von der Leyen, alitangaza kampeni ya kimataifa kupitia juhudi za Poland ya kuwatafuta na kuwarudisha nchini Ukraine watoto waliosafirishwa kwa nguvu nchini Urusi.