1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Rais wa zamani wa Kosovo akanusha mashitaka ya uhalifu

4 Aprili 2023

Rais wa zamani wa Kosovo Hashim Thaci pamoja na viongozi wengine watatu wa jeshi la ukombozi la Kosovo KLA wamekanusha mashitaka ya uhalidu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita

https://p.dw.com/p/4Pfpe
Den Haag Prozess gegen Ex-UCK Anführer Hashim Thaci
Picha: Koen van Weel/REUTERS

Waendesha mashitaka wameiambia mahakama hiyo siku ya kwanza ya kusikilizwa kwa kesi hiyo hapo jana kwamba rais wa zamani wa Kosovo aliongoza kampeni ya mauaji na mateso dhidi ya wapinzani wakati wa vita vya kupigania uhuru kutoka kwa Serbia kati ya 1998 na 1999.

Thaci alithibitisha rufaa aliyoiwasilisha wakati alipofika mbele ya mahakama hiyo kwa mara ya kwanza 2020 na akasema hana hatia. Waandamanaji waliandama huko The Hague kumuunga mkono Thaci ambaye alistaafu mnamo 2020 na amekuwa akizuiliwa na mahakama hiyo tangu wakati huo.

Maalfu ya waandamanaji wengine waliandamana mjini Pristina kabla kuanza kwa kesi hiyo.