Rais wa zamani wa Haiti arudi Karibiki:
16 Machi 2004Matangazo
KINGSTON: Wiki mbili baada ya kulazimia kujiuzulu, Rais wa zamani wa Haiti, Jean-Bertrand Arsistide amerudi eneo la Karibiki, Amewasili kisiwani Jamaika ambako alisema atabakia kwa muda wa wiki nane hadi kumi kwa niya ya kuwazuru jamaa zake na kutafuta nchi itakayompa himaya ya kisiasa. Kama hatua ya kulalamika dhidi ya ziara hiyo, Waziri Mkuu wa Haiti Gerard Latortue amemrejesha nyumbani balozi wake mjini Kingston na kuvunja kwa muda uhusiano wa kibalozi na Jamaika. Nayo Marekani imetiwa wasi wasi na ziara hii ya Aristide. Serikali mjini Washiongton imesema inakhofia kwenda kwake Jamaika kunaweza kuchochea tena mapigano ya umwagaji damu nchini Haiti.