SiasaUrusi
Uturuki na Japan zazungumzia mkataba wa Bahari Nyeusi
9 Septemba 2023Matangazo
Mapema mwezi huu, Erdogan alisema kuwa, baada ya majadiliano yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kuna uwezekano wa kuufufua mkataba huo wa nafaka.
Urusi ilijiondoa katika mkataba wa usafirishaji nafaka
Urusi ilijiondoa katika mkataba huo uliokuwa ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki kutokana na malalamiko kuwa usafirishaji wa bidhaa zake za vyakula na mbolea ulikuwa ukikabiliwa na vikwazo. Ilisema pia kwamba nafaka za Ukraine hazikuwa zikipelekwa katika nchi zenye uhitaji.