1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani Steinmeier ziarani Afrika Kusini

Oumilkheir Hamidou
19 Novemba 2018

Rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameanza ziara rasmi ya siku nne itakayomfikisha Afrika Kusini na baadae Botswana. Kituo cha kwanza ni Johannesburg kabla ya kuondoka kwenda Cape Town

https://p.dw.com/p/38XS0
Bundespräsident Steinmeier in Südafrika
Picha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

 Katika ziara hiyo rais wa shirikisho Steinmeier amefuatana na ujumbe mkubwa wa wanauchumi. Lengo la mazungumzo yake pamaoja na viongozi wa Afrika Kusini ni kuimarisha ushirikiano pamoja na mshirika muhimu zaidi wa Ujerumani barani Afrika. Afrika Kusini ni nchi pekee ya bara la Afrika katika kundi la mataifa 20 yaliyoendelea kiviwanda na yale yanayonyanyukia kiuchumi ulimwenguni-G-20.

Akianza ziara hiyo mjini Johannesburg rais Steinmeier ameisifu Afrika Kusini na kuitaja kuwa nchi ya "mapambazuko na fursa ya maana kwa Ujerumani." Nchi inapata sifa kutokana na  ufanisi wake katika juhudi za kupambana na rushwa" ameongeza kusema.

 

Nelson Mandela akiwapongeza wana rugby wa Afrika Kusini-Springbok
Nelson Mandela akiwapongeza wana rugby wa Afrika Kusini-SpringbokPicha: Getty Images/AFP/J.P. Muller

Nelson Mandela ni mfano mzuri wa kiongozi na binaadam

Amemsifu pia mpigania uhuru wa Afrika Kusini,Nelson mandela na kumtaja kuwa "kitambulisho kilicho ng'ara cha suluhu na utu." Mandela alikuwa mfano wa kuigizwa kama kiongozi na pia kama binaadam" amesisitiza katika hotuba aliyotoa katika jengo la makumbusho dhidi ya ubaguzi na mtengano Apartheid. "Afrika Kusini imeipatia funzo Ujerumani kwamba demokrasia haipatikana hivi hivi. Demokrasia ni matunda ya moyo wa kijasiri . Amewahimiza waafrika Kusini watekeleze ndoto ya Nelson Mandela ya kuwa na "dola la upinde wa mvuwa."

Rais Steinmeier ametilia mkazo azma ya Ujerumani ya kuwa mshirika wa kimataifa katika haki za binaadam, amani na dhidi ya hisia kali za kizalendo. Ametetea umuhimu wa ushirikiano kati ya Ulaya na bara la Afrika, kipa umbele kikiwa "uwekezaji, ajira na aina mpya ya ushirikiano.

Rais Steinmeier akizuru mnara wa Ponte mjini Johannesburg
Rais Steinmeier akizuru mnara wa Ponte mjini JohannesburgPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

 Rais Steinmeier amepangiwa kukutana na rais Ramaphosa

Kabla ya hapo rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani na ujumbe aliofuatana nao walikutana na wawakilishi wa kiuchumi mjini Johannesburg. Kesho rais wa shirikisho atakwenda Cape Town ambako amepangiwa kuzungumza na rais Cyril Ramaphosa. Atahudhuria pia katika sherehe za kutiwa saini mkopo kwaajili ya sera za kueneza maji safi katika jiji la Cape Town kutoka taasisi ya Ujerumani ya mikopo ya ujenzi mpya.

Jumatano rais Steinmeier ataondoka Afrika Kusini kwenda Botswana ambako amepangiwa kukutana na rais Mokgweetsi Masisi mjini Gabarone kaabla ya kurejea Beli9n aalkhamisi inayokuja.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/KNA/dpa

Mhariri:Yusuf Saumu