Rais wa Tunisia Saied aapishwa kwa muhula wa pili
23 Oktoba 2024Wiki kadhaa baada ya kushinda tena uchaguzi kwa asilimia 97 ya kura, profesa huyo wa zamani wa sheria mwenye umri wa miaka 66 katika hotuba yake ya kuapishwa ametoa wito wa kile alichokiita mapinduzi ya kitamaduni ili kupambana na ukosefu wa ajira, vita dhidi ya ugaidi na kuangamiza ufisadi. Saied amesema katika hotuba yake kwa wabunge wa Tunisia kuwa lengo ni kuijenga nchi ambayo kila mmoja anaweza kuishi kwa heshima. Ushindiwa Saied katika uchaguzi wa Oktoba 7 ulijiri baada ya muhula wa kwanza wenye misukosuko amnapo alilivunja bunge la nchi hiyo, akaiandika upya katiba iliyoidhinishwa baada ya wimbi la mapinduzi ya umma lililopiga ulimwengu wa Kiarabu na akawafunga jela wakosoaji wake wa kisiasa, vyombo vya habari, biashara na asasi za kiraia.