Rais wa Tunisia akataa masharti ya IMF kuhusu mkopo
6 Aprili 2023Rais wa Tunisia Kais Saied amesema hivi leo kuwa hakubaliani kabisa na masharti ya Shirika la Fedha Ulimwenguni, IMF, kuhusu mpango wa dola bilioni 1.9 wa kuisaidia nchi hiyo, huku akionya kuwa kupunguzwa kwa ruzuku ya chakula na nishati kunaweza kusababisha machafuko.
Septemba mwaka jana, Tunisia ilifikia makubaliano ya mkopo na IMF, lakini hadi sasa mkopo huo haujatolewa kwa kuwa wafadhili wanaamini kuwa hali ya fedha nchini humo inaendelea kutofautiana na takwimu na mahesabu ya awali ya mpango huo.
Rais Saied amekumbushia ghasia zilizoitikisa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini mnamo mwaka 1983 baada ya serikali kupandisha bei ya mkate, huku akisema kuwa amani ya umma si jambo la mzaha. Tunisia inakabiliwa na matatizo ya fedha na imekua ikishindwa kulipa madeni yake ya ndani na nje ya nchi.