Rais wa Somalia amelazwa hospitali Kenya
5 Desemba 2007Matangazo
Rais wa Somalia,Abdullahi Yusuf amelazwa hospitali mjini Nairobi huku habari zikitatanisha kuhusu hali yake.Balozi wa Somalia nchini Kenya, Mheshimiwa Mohamed Ali Nur amesema,Rais Yusuf anafanyiwa uchunguzi wa kawaida kabla ya kuelekea London.Wakati huo huo,alikanusha habari zilizosema kuwa hali ya kiongozi huyo ni mbaya.