Rais wa Senegal anazitembelea Mali na Burkina Faso
30 Mei 2024Faye alitua kwenye uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Mali, Bamako leo mchana na alipangiwa kufanya mazungumzo na kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo Kanali Assimi Goita.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Senegal imesema ziara kama hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano ya jadi na ya kidugu baina ya mataifa hayo.
Soma pia:Kiongozi wa Senegal aombwa kusaidia kutatua mivutano iliyopo ECOWAS
Tangu alipoapishwa mapema mwezi April, Faye amekwishafanya ziara kadhaa kwenye mataifa ya magharibi mwa Afrika. Safari yake ya leo mjini Bamako na baadaye kwenye mji mkuu wa Burkina Fasso, Ougadogou itakuwa ya tisa.
Kiongozi huyo aliyeshinda urais katika uchaguzi wa kihistoria nchini Senegal ameahidi kufanya kila awezalo kuzishawishi Mali, Burkina Faso na Niger zinazotawaliwa kijeshi kurejea ndani ya jumuiya yaECOWAS.