Rais wa Poland ana corona, awaomba radhi aliokaribiana nao
24 Oktoba 2020"Napenda kuwaomba radhi wote waliowekwa chini ya utaratibu wa kukaa karantini kwa sababu ya kukutana na mimi katika siku za karibuni," alisema rais Andrzej Duda. "Iwapo ningekuwa na dalili zozote, niaminini, mikutano yote ingefutwa.
Vipimo vya Duda vinakuja wakati kukiwa na ongezeko kubwa la visa vipya vilivyothibitishwa vya covid-19 na vifo vinavyohusiana na virusi hivyo nchini Poland, taifa la watu milioni 38 lililoshuhudia maambukizi kidogo sana katika msimu wa machipuko.
Soma pia: Maambukizi ya Corona yaongezeka Ulaya na Amerika Kusini
Majukumu muhimu ya kitaasisi ya rais huyo, yanajumlisha kuongoza sera ya kigeni na kusaini sheria. Lakini mengi ya majukumu yake si ya kimamlaka, na majukumu mengi zaidi ya kuendesha nchi yako chini ya serikali ya waziri mkuu Mateusz Morawiecki.
Jumamosi Poland iliripoti visa vipya 13, 628 na rekodi ya vifo 179 vya siku moja kutokana covid-19. Idadi ya visa vya kila siku ilikuwa ya pili kwa ukubwa kitaifa katika janga hilo baada ya rekodi ya idadi iliyowekwa siku ya Ijumaa. Mizozo ya kijamii pia inongezeka nchini humo.
Polisi ilitumia gesi ya kutoa machozi Jumamosi dhidi ya waandamanaji waliokasirishwa na vikwazo vya kirusi hicho, ambao walikuwa kundi linalojumlisha wajasiriamali, wanasiasa wa mrengo mkali wa kulia, mashabiki wa soka na wapinzani wa chanjo. Waandamanaji hao, wengi wao wakiwa hawana vifaa vyote vya kinga, walivunja kikomo cha mikutano ya umma.
Som pia: Rais wa Poland Andrzej Duda, aibuka kidedea uchaguzi wa rais
Wakosoaji wanakituhumu chama tawala cha mrengo mkali wa kulia kwa kutumia kisingizio cha janga na mahakama kiliyoijaza na watiifu kuzuwia upatakinaji wa huduma za utoaji mimba kwa njia tata za kisheria.
Wanakituhumu pia cham cha Sheria Haki kwa kutaka kuchochea mizozo ya kijamii ili kuondoa nadhari kwenye viwango vinavyoongezeka vya maambukizi ya Covid-19.
Chanzo: APE