1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Peru aondolewa madarakani

8 Desemba 2022

Bunge la Peru limemuondoa madarakani Rais Pedro Castillo na nafasi yake kuzibwa na makamo, Dina Boluarte muda mfupi baada ya Castillo kujaribu kulivunja bunge hilo, ikiwa kabla ya zoezi la kumpigia kura ya kumwondoa.

https://p.dw.com/p/4KdSi
Peru I Vereidigung der peruanischen Vizepräsidentin Boluarte
Picha: Sebastian Castaneda/REUTERS

Ofisi maalumu yenye kuhusika na masuala ya uchunguzi nchini humo ilisema kitendo cha Castillo anaehusishwa na kupoteza udalifu kazini cha kujairibu kulivunja bunge ni sawa na tukio la mapinduzi.

Walipiga kura za ndio 101 na hapana 6 huku kura 10 kutokuwepo. Muda mfupi kabla ya kupigwa kwa kura hizo Castillo alitanga kuweka serikali ya dharura na kutaka duru ya pili ya mkutano wa bunge ya kufanikisha katiba mpya taifa hilo.

Marekani yaipongeza Peru kwa umadhubuti wa taasisi zake

Peru I Präsident Kongress
Wabunge wakishanglia kumuonda Rais Pedro Castillo Picha: Guadalupe Pardo/AP/picture alliance

Katika hatua nyingine serikali ya Marekani ilisema imeupokea vyema  uteuzi wa Bibi Boluarte kama Rais wa Peru, ambaye tayari ameapishwa na bunge la taifa hilo katika siku ambayo kulishuhudiwa kiongozi wa aliyeondolewa Castillo akitiwa nguvuni baada ya kufurushwa mamlakanai.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imepongeza umadhubuti wa taasisi za Peru kwa kuhakikisha umadhubuti wa kidemokrasia na itaendelea kuliunga mkono taifa hilo chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Soma zaidi:Peru inaongoza kwa kasi kubwa ya vifo vya Covid-19

Bibi Boluarte, mwanasheria mwenye umri wa miaka 60, atakuwa mwanamke wa kwanza kufikia ngazi ya urais nchini Peru,ikiwa tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Chanzo: RTR