1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Msumbiji ziarani nchini Tanzania

11 Januari 2021

Rais wa Msumbiji na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, Filipe Nyusi, ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania ambapo amekutana na mwenyeji wake Rais John Magufuli kwenye wilaya ya Chato mkoani Geita.

https://p.dw.com/p/3nn3l

Ziara hiyo itaangazia masuala mbalimbali kati ya mataifa hayo mawili, ikiwemo demokrasia na biashara. 

Ziara ya Rais Nyusi imetanguliwa na shughuli ya kijamii ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa hospital ya Rufaa ya Chato.

Mosambik | Provinz Nampula | Vertriebene Kinder Opfer von Terrorismus
Hali ya usalama ni tete kwenye jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Cabo Delgado Picha: Roberto Paquete/DW

Mapema mwezi Mei, mwaka 2020 Tanzania ilipeleka vikosi vyake kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Msumbiji kama hatua ya tahadhari baada ya kutokea machafuko katika jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji yanayofanywa na wanamgambo ambao wamekuwapo tangu mwaka 2017.

Aidha, mwishoni mwa mwaka 2020 kuliibuka taarifa za uwepo wa watu waliotajwa kuvuka mipaka kutoka Msumbiji na kuingia mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania na kutekeleza matukio ya uhalifu.

Usalama wa mipaka ndiyo kitovu cha majadiliano 

Afrika Tansania Mosambik SADC  John Magufuli
Rais John Magufuli wa Tanzania Picha: DW/D. Khamis

Marais hao wawili watatumia ziara hiyo kwa kufungua mazungumzo yatakayolenga kuimarishwa kwa masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mipaka kwa nchi zote mbili na usalama kwa raia.

Ziara ya Rais Nyusi hapa nchini Tanzania mbali na kujadiliana juu ya masuala ya kiusalama kati ya mataifa haya mawili, pia imelenga kufungua mipaka ya kiashara kati ya Msumbiji na Tanzania kwa hususan malighafi kutoka ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Ziara ya Rais Nyusi inafanyika miezi michache tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirrokutoa taarifa ya kukamatwa kwa waliotajwa kuwa watu waliohusishwa na vitendo vya kigaidina kutekeleza matukio ya uhalifu katika kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara.

Tanzania na Msumbiji zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara na kiutamaduni na kumekuwa na maingiliano ya kibiashara na hata kijamii kati ya wananchi wa mataifa hayo mawili, hususan kwenye eneo la kusini mwa Tanzania.