1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Msumbiji awatimua mawaziri sita serikalini

3 Machi 2022

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafuta kazi mawaziri wake sita, akiwemo waziri wa fedha wa nchi hiyo, katika kile kinachoonekana kuwa mabadiliko makubwa ya baraza la mawawiri.

https://p.dw.com/p/47wSN
Ossufo Momade lider da Renamo und Filipe Jacinto Nyusi
Picha: Roberto Paquete/DW

Taarifa fupi iliyotolewa na ofisi ya rais ilisema ametumia mamlaka yake ya kikatiba kuwaachisha kazi mawaziri hao wa serikali yake. 

Hata hivyo haikutoa sababu yoyote ya kutimuliwa kwa mawaziri hao, wala kutangaza uteuzi wowote mpya au ishara ya ni lini nyadhifa zao zitajazwa.

Mawaziri wa ngazi ya juu waliofutwa kazi ni pamoja na Adriano Afonso Maleiane, waziri wa Fedha na Uchumi, na Ernesto Max Elias Tonela, Waziri wa Raslimali za Madini na Nishati.

Chanzo: reuters