1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Mexico awasilisha ripoti kuhusu utendaji wa serikali

Josephat Charo
2 Septemba 2024

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador amewaaga wafuasi wake anapojiandaa kukabidhi madaraka kwa rais mpya.

https://p.dw.com/p/4kA93
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez ObradorPicha: Raquel Cunha/REUTERS

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador amewasilisha ripoti yake ya mwisho akitetea kipindi cha utawala wake mwezi mmoja kabla kukabidhi madaraka kwa mrithi wake Claudia Sheinbaum wa chama chake cha Morena.

Katika uwanja wa Zacalo katikati ya mji wa Mexico, Lopez Obrado amewaaga maelfu ya wafuasi wake huku akiungwa mkono kwa asilimia 73 wakati muhula wake wa miaka sita ukielekea mwisho.

Katika hotuba iliyodumu kipindi cha masaa mawili Lopez Obrador amesema raia wa Mexico wanaishi katika demokrasia ya kweli, kujenga nchi mpya na kuweka misingi ya kuanza awamu mpya.

Ripoti ya rais ni utamaduni katika siasa za Mexico wa tathmini ya mwaka ya mafanikio ya serikali tofauti ya hotuba kuhusu hali ya taifa inayotolewa na rais wa Marekani. Rais Lopez Obrador atakabidhi madaraka kwa Sheinbaum Oktoba mosi.