1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Biden kupigia upatu uhuru na demokrasia Ufaransa

7 Juni 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anayeendelea na ziara yake nchini Ufaransa anatarajiwa kupigia upatu demokrasia katika hotuba yake muhimu mbele ya viongozi wengine wa nchi za Magharibi huko Normandy.

https://p.dw.com/p/4gnop
Paris, Ufaransa | Marekani | Rais Joe Biden na Emmanuel Macron
Rais wa Marekani Joe Bide akiwa na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Jim Watson/AP/picture alliance

Sehemu ya hotuba hiyo iliyochapishwa na ikulu ya White house na kunukuliwa na vyombo vya habari,rais Biden amesema mapambano ya kupigania demokrasia ni magumu na yanaanza na kila mmoja.

Soma pia:D-Day: Macron, Biden wakutana na Zelensky

Biden ataitowa hotuba yake kama sehemu ya muendelezo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu vikosi vya Marekani na nchi washirika kuanzisha operesheni ya kuikomboa ulaya dhidi ya Ujerumani iliyokuwa ikitawaliwa na Wanazi,katika kile kinachoitwa D Day.

Kabla ya kuelekea Normandy Biden alifanya mazungumzo na rais Emmanuel Macron katika kasri la Elysee lakini pia alizungumza na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky .

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW