1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki ataka haki zilindwe

14 Januari 2022

Rais mpya wa Mahakama ya Afrika inayoshughulika na haki za binadamu yenye makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania Jaji Imani Aboud, ametoa wito wa kulindwa kwa haki za binadamu, akisema bado haki hizo zinavunjwa.

https://p.dw.com/p/45Wvy
Hammer Gerichtssaal Gericht Richter-Hammer
Picha: Adrian Wyld/empics/picture alliance

Rais mpya wa Mahakama ya Afrika inayoshughulika na haki za binadamu yenye makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania Jaji Imani Aboud, ametoa wito wa kulindwa kwa haki za binadamu, akisema bado haki hizo zinavunjwa na kuuweka mashakani uhuru wa demokrasia katika nchi nyingi za Afrika.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa maalumu kama salamu za mwaka mpya, Jaji Aboud amesema ni lazima kuwe na uwajibikaji wa kulinda na kutekeleza haki za binadamu kwa serikali za nchi za Afrika na mashirika ya kiraia yanayotetea haki za binadamu.

Amesema kuwa mahakama pekee haiwezi kujitosheleza kama mifumo ya nchi ya kulinda haki haijawa imara.

Rais huyo raia wa Tanzania ambaye pia ni jaji wa Mahakama Kuu nchini humo, amesisitiza kwamba mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea katika nchi za Afrika, yanahitaji taasisi imara na huru ambazo haziingiliwi na mamlaka za kiserikali ili kuleta imani kwa umma.