1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Israel Herzog ahudhuria Kongamano la Kiuchumi Davos

18 Januari 2024

Rais wa Israel Isaac Herzog na mkuu wa kampuni ya mtandao wa ChatGPT wanahudhuria Kongamano la Kiuchumi Duniani, katika siku ya tatu ya mkutano huo wa kila mwaka unaofanyika Davos, Uswisi.

https://p.dw.com/p/4bPWt
Israel/ Herzog
Rais wa Israel Isaac HerzogPicha: Nicolas Messyasz/abaca/picture alliance

Rais Herzog anatarajiwa kuzungumzia hali ya mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas tangu ule uvamizi wa Oktoba 7 uliofanywa nchini Israel.

Herzog amesema anafahamu kwamba janga la kibinadamu linafanyika Gaza ila ni sharti Israel ijilinde dhidi ya ugaidi.

Jukwaa la Uchumi Duniani la Davos kuanza leo

Dunia kwa sasa inatazama idadi ya vifo vinavyoongezeka Gaza kufuatia kampeni ya kijeshi ya Israel inayolenga kuwaangamiza wanamgambo waliojihami wa Hamas.

Mtaalam mmoja wa afya wa Umoja wa Mataifa amesema Wapalestina wanafariki kila siku Gaza katika hospitali zilizolemewa na mzigo wa majeruhi, kutokana na masjhambulizi ya Israel.