RAIS WA IRAN :MAREKANI SI MPATANISHI LEBANON
6 Agosti 2006Matangazo
TEHERAN:
Rais Ahmadinejad wa Iran amezitoa thamani juhudi za amani za Marekani katika mgogoro unaoendelea nchini Lebanon kwa kuwa Marekani imeelemea upande mmoja ikiungamkono Israel.Katika mtandao wake, rais wa Iran amenukuliwa kusema, „Marekani inayoungamkono dola la kizayuni hadi leo , haina haki kujiingiza katika mzozo huu kama mpatanishi.